Israel yauwa wanamgambo kadhaa wa Kipalestina | Habari za Ulimwengu | DW | 28.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Israel yauwa wanamgambo kadhaa wa Kipalestina

GAZA CITY

Wafanyakazi wa hospitali katika Ukanda wa Gaza wanasema wanamgambo watano wa Kipalestina wameuwawa katika mashambulizi mawili tafauti ya Israel.

Wanaume watatu wawili kutoka kundi la itikadi kali za Kiislam la Jihad na mmoja kutoka kundi la Hamas wameuwawa karibu na mji wa kusini wa Khan Younis.Watu wengine sita wamejeruhiwa.

Jeshi la Israel limesema mashambulizi yao yamelenga wapiganaji wanaofyetuwa maroketi na mizinga dhidi ya Israel.

Muda mfupi baadae wanamgambo wawili wa kundi la Jihad waliuwawa na wengine wawili kujeruhiwa katika shambulio la anga katikati ya Ukanda wa Gaza.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com