Israel yaendelea kushambulia Ukanda wa Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 01.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Israel yaendelea kushambulia Ukanda wa Gaza

GAZA:

Zaidi ya Wapalestina 20 wameuawa katika mashambulizi mapya yaliyofanywa na majeshi ya Israel katika Ukanda wa Gaza.Watoto 3 ni miongoni mwa wale waliouawa.Wizara ya afya inayoongozwa na Hamas katika mji wa Gaza imesema majeshi ya anga na nchi kavu ya Israel yameushambulia mji wa Jabalia.

Kwa mujibu wa jeshi la Israel,operesheni hiyo ililenga miundo mbinu ya magaidi katika Ukanda wa Gaza.Msemaji wa jeshi amesema,wanamgambo wa Kipalestina kwa mara nyingine tena wamerusha makombora katika ardhi ya Israel na watu 3 walijeruhiwa kidogo katika mji wa Aschkelon.

Tangu Muisraeli mmoja alipouawa na kokombora lililorushwa na Wapalestina siku ya Jumatano,kiasi ya Wapalestina 50 wameuawa katika mapigano na mashambulizi ya jeshi la anga la Israel kwenye Ukanda wa Gaza.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com