1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel na Palestina zaalikwa katika mkutano wa amani.

21 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CQ6O

Washington. Marekani imethibitisha kuwa itakuwa mwenyeji wa mkutano wa amani ya mashariki ya kati wiki ijayo wenye lengo la kuanzisha upya majadiliano ya kuundwa kwa taifa la Palestina. Mialiko imetolewa kwa Israel , Palestina , umoja wa mataifa na mataifa muhimu ya Kiarabu kama Saudi Arabia na Syria. Lakini Marekani bado inajaribu kuyashawishi mataifa ya Kiarabu kutuma wawakilishi wao.

Mkutano huo utakaofanyika Novemba 27 , katika chuo cha jeshi la majini la Marekani kilichoko Maryland, utakuwa mkutano wa kwanza wa majadiliano kuhusu amani ya mashariki ya kati tangu mwaka 2000. Kabla ya mkutano huo , rais wa Marekani George W. Bush atakuwa na mazungumzo ya pamoja na rais wa Palestina Mahmoud Abbas na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert mjini Washington.