Israel itawacha ujenzi kwenye Ukingo wa Magharibi? | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 15.09.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Israel itawacha ujenzi kwenye Ukingo wa Magharibi?

Viongozi wa Israel na Palestina wameshindwa kufikia makubaliano yoyote katika suala la ujenzi wa makazi ya Wayahudi kwenye Ukingo wa Magharibi.

Benjamin Netanyahu,Hillary Clinton na Mahmoud Abbas

Benjamin Netanyahu,Hillary Clinton na Mahmoud Abbas

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas walikutana Sharm-el Sheikh nchini Misri katika awamu ya pili ya mazungumzo ya ana kwa ana yaliyo na azma ya kuisaka amani ya kudumu ya Mashariki ya Kati.Hata hivyo,mjumbe maalum wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati George Mitchell anasisitiza kuwa msimamo wao kuhusu suala hilo haujabadilika.

Barack Obama mit Benjamin Netanyahu und Mahmoud Abbas NO FLASH

Viongozi wa Israel na Palestina walipokutana Washington kwa mara ya kwanza ana kwa ana baada ya zaidi ya mwaka mmoja.

Mjumbe huyo aliendelea kueleza kuwa mazungumzo hayo sharti yapewe uzito na yawe ya faragha.Itakumbukwa kuwa muda uliowekwa wa kuusitisha ujenzi wa makazi ya Wayahudi katika Ukingo wa Magharibi utamalizika mwishoni mwa mwezi huu.Kwa upande wake Rais Mahmoud Abbas ametoa vitisho kuwa huenda akajiondoa kwenye meza ya mazunguzumzo endapo ujenzi huo utaanza tena upya.Hii leo,Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton anatazamiwa kukutana na wawakilishi wa Israel na Palestina kwenye kikao cha pamoja kitakachofanyika mjini Jerusalem.

DW inapendekeza

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com