ISLAMABAD : Musharraf akataa ashinikizo la Bhutto | Habari za Ulimwengu | DW | 30.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD : Musharraf akataa ashinikizo la Bhutto

Rais Generali Pervez Musharraf wa Pakistan amekataa shinikizo lolote lile au kuwekewa muda wa mwisho kuamuwa iwapo au la an’gatuke kwenye wadhifa wa mkuu wa majeshi baada ya kiongozi wa upinzani Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto kudai kwamba kiongozi huyo atajiuzulu kwenye wadhifa huo chini ya makubaliano ya kurudisha demokrasia nchini Pakistan.

Generali huyo mshirika wa Marekani na waziri mkuu huyo wa zamani wa Pakistan wako kwenye mazungumzo ya kufikia makubaliano ya kushirikiana madaraka na upinzani ambayo yatakomesha utawala wa kijeshi wa miaka minane nchini humo baada ya Musharraf kutwaa madaraka katika mapinduzi ya kijeshi.

Maafisa wa serikali hawakuweza kupatikana mara moja au wamekataa kuzungumzia moja kwa moja juu ya kauli ya Bhutto hapo jana kwamba Musharraf alikuwa tayari ameamuwa kuacha wadhifa huo mkubwa wa kijeshi wenye nguvu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com