1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Iran yawaita mabalozi wake wa Ujerumani, Ufaransa, Uingereza

27 Septemba 2025

Iran imewarejesha nyumbani mabalozi wake katika nchi za Ujerumani, Ufaransa na Uingereza ili kufanya mashauriano kuhusu mgogoro wa mchakato wa Umoja wa Mataifa ulioanzishwa na nchi hizo wa kuirejeshea tena vikwazo Tehran

https://p.dw.com/p/519MK
Iran inakabiliwa na hatari ya kuwekewa tena vikwazo na Umoja wa Mataifa
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian akizungumza mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa 24.09.2025Picha: Michael M. Santiago/Getty Images/AFP

Hatua ya kuwarejesha nyumbani wawakilishi hao wa kidiplomasia Iran imechukuliwa saa kadhaa baada ya juhudi za Urusi na China za kuchelewesha kufufua vikwazo dhidi ya Iran kugonga mwamba Ijumaa mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Hofu ya Umoja wa Mataifa kuiwekea tena vikwazo Iran

Hayo yanajiri wakati Umoja wa Mataifa ukitazamiwa kuiwekea vikwazo vikali Iran Jumamosi  27.09.2025 baada ya mazungumzo ya nyuklia kati ya taifa hilo na mataifa ya magharibi kukwama. Vikwazo hivyo vitakapotangazwa vinatazamiwa kuanza kufanya kazi kuanzia Jumapili.