Irak yanyakua Kombe la Asia | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 29.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Irak yanyakua Kombe la Asia

Irak imeshinda Kombe la Asia,baada ya kuikandika Saudi Arabia mkwaju mmoja kwa bila katika fainali iliyochezwa mji mkuu wa Indonesia,Jakarta.

Mashabiki wa Kiiraki na bango linalosemaVita havikuweza kuuwa kandanda

Mashabiki wa Kiiraki na bango linalosema"Vita havikuweza kuuwa kandanda"

Hapo kabla,kocha wa Irak,Jorvan Viera alisisitiza umuhimu wa mchezo huu kwa wachezaji wake na nchi yao katika wakati huu wa ghasia za kisiasa nchini Irak.Alisema:

„Huenda ikawa wataweza kuyakaweka kando matatizo ili waweze kucheza mpira na kuwafurahisha wenzao nyumbani na kuwapatia sababu ya kutabasamu.“

Kwa upande mwingine maafisa nchini Irak wamepiga marufuku magari kutembea barabarani katika mji mkuu Baghdad na miji ya Kirkuk,Nadjaf na Kerbala. Kwa mujibu wa msemaji wa kijeshi wa ngazi ya juu, hatua hiyo imechukuliwa ili kuzuia mashambulizi dhidi ya washabiki wa kandanda waliokuwa wakifurahia Iraq kuingia katika fainali ya Kombe la Asia dhidi ya Saudi Arabia katika mji mkuu wa Indonesia,Jakarta.

Mapema juma lililopita hadi watu 50 waliuawa na zaidi ya 100 wengine walijeruhiwa katika mashambulizi mawili ya mabomu ya gari yaliolenga washabiki waliokuwa wakisherehekea ushindi wa Irak,baada ya kuifunga Korea ya Kusini katika nusu fainali.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com