1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano Iran

Sekione Kitojo29 Desemba 2009

Baada ya kutokea machafuko yaliyomwaga damu nchini Iran utawala wa nchi hiyo kwa miezi kadha sasa unaendelea na matumizi ya nguvu dhidi ya wakosoaji wake.

https://p.dw.com/p/LFzn
Waandamanaji wakiandamana , wakionyesha upinzani wao kwa serikali ilikuwa tarehe 12. Juni 2009,mjini Berlin mbele ya ubalozi wa Iran.Picha: AP

Baada ya kutokea machafuko yaliyomwaga damu nchini Iran utawala wa nchi hiyo kwa miezi kadha sasa unaendelea na matumizi ya nguvu dhidi ya wakosoaji wake. Jana Jumatatu kumetokea tena mapambano kati ya waandamanaji na polisi. Viongozi kadha maarufu wa upinzani wamekamatwa. Lakini pamoja na mapambano hayo, huwezi kutarajia kuwa maandamano hayo ya upinzani yanaongezeka. Ni kinyume chake.

Miezi sita baada ya uchaguzi wa rais uliobishaniwa, maandamano ya upinzani hayajakoma, yanaongezeka nguvu zake kila inapotokea nafasi. Kumekuwa na mapambano makali kabisa hivi karibuni mjini Tehran pamoja na miji mingine ya nchi hiyo, na hata serikali ya Iran haikuweza tena kuficha , kwamba waandamanaji walipigwa risasi, na mmoja wao ni mpwa wa kiongozi wa upinzani Mir Hossein Mousavi, mwenye umri wa miaka 41.

Idadi ya watu waliojeruhiwa na wale waliokamatwa haifahamiki kama ilivyo kwa uharibifu mkubwa uliotokea, ikiwa serikali ya nchi hiyo imeweka udhibiti mkubwa kwa taarifa zinazotoka nje, lakini kutokana na picha zinazoonyesha uharibifu, magari yaliyochomwa moto, pikipiki pamoja na maduka, picha ambazo zinatolewa na televisheni ya taifa, zinaonyesha hali ambayo si tulivu na jinsi mapambano hayo yalivyokuwa makubwa.

Hii ikiwa na maana kuwa hali hiyo ya mapambano inaelekea katika hali mbaya zaidi ya kulipuka. Inaonyesha wakati wote kunapokuwa na tatizo wanaharakati za maandamano wanahamasisha watu kuingia mitaani, na raia wanaitikia wito.

Kichocheo cha ghasia za hivi karibuni ni maadhimisho ya sikukuu ya Ashura ambapo Washia wanakumbuka kifo cha mjukuu wake Mtume Muhammad, Hossein ambaye aliuwawa kikatili. Jamii inaonyesha hisia zake kwa maumivu hayo aliyoyapata katika siku hii muhimu ya maombolezo kwa Washia ikiwa imechanganyika na maadhimisho ya ayatollah mkuu Ali Montazeri wiki moja iliyopita, mmoja kati ya waasisi wa mapinduzi ya Kiislamu lakini wakati huo huo amekuwa akiunga mkono maandamano.

Kwa hali yoyote ile dini, ikiwa ni kiini cha harakati za upinzani inajionyesha kuwa kwa kiasi kikubwa inarithi masuala haya yote mawili na inaonyesha kuwa ni sababu ya kuzuka kwa maandamano. Ambapo kwa sehemu ya waandamanaji wanataka kuuondoa uongozi wa Kiislamu na wengine wanataka kuudhoofisha utawala wa Tehran, pengine kwa msaada wa mataifa ya nje.

Iwapo hilo ni sahihi, basi itakuwa ni watu wachache sana. Na hili hata maafisa nchini humo wanalifahamu. Licha ya mapambano makali, ongezeko la watu kukamatwa na kesi kufunguliwa, hakutakuwa na mapambano makubwa zaidi. Hawajamkamata hata mara moja kiongozi maarufu wa upinzani Mir-Hossein Moussavi na wanasita bila shaka, na wamegawanyika kuhusiana na jinsi ya kulishughulikia suala.

Suala moja ni hakika hapa, kwamba viongozi mjini Tehran kwa muda mrefu wanafahamu , kuwa hali ya kutoridhika haiwawezi kuizuwia kutoka kwa waandamanaji, badala yake liko katika eneo kubwa la raia. Lakini hawafahamu pia, cha kufanya. Kila mapambano mapya yanaifanya hali kuwa mbaya zaidi na huenda muda umekwisha pita, kwa ushauri wa spika wa bunge Larijani kuweza kutumiwa na matatizo ya waandamanaji kujadiliwa.

Mwandishi : Peter Philipp/ ZR / Sekione Kitojo

Mhariri : Yusuf Saumu