1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matamshi ya chuki

Ni matamshi yenye maudhui ya kuumiza yenye lengo la kushambulia mtu mmoja mmoja ama kundi la watu. Yanahusisha aina zote za matamshi, yakiwemo ya kuandika, ishara au maoni yaliowekwa kwenye mitandao ya kijamii.

Matamshi ya chuki yanayochapishwa mtandaoni huwa yanawalenga watu wa jamii za wachache, wakiwemo wanawake, watu wenye mahitaji maalumu au wageni. Zaidi ya hapo, yanalenga pia dini, rangi au itikadi. Kwa kawaida matamshi ya chuki yanamtishia mtu au kundi la watu na kuhamasisha tabia ya vurugu. Hatua za kisheria dhidi ya matamshi ya chuki zinatofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine. Mwaka 2016 kampuni za Facebook, Google, Microsoft na Twitter zilikubaliana kuhusu kanuni za maadili za Umoja wa Ulaya zinazotaka maudhui nyingi za chuki kufutwa ndani ya muda wa masaa 24 baada ya kuchapishwa. Ujerumani ni moja ya mataifa ambako matamshi ya chuki yanaweza kushtakiwa katika kesi za kukashifu, uchochezi na udhalilishaji. Ukurasa huu ni mkusanyiko wa maudhui za DW kuhusu matamshi ya chuki.

Onesha makala zaidi