1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA: Shirika la kimataifa la usafiri wa anga latupilia mbali pendekezo la Marekani-

30 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFng



Shirika la kimataifa la usafiri wa anga, limetupilia mbali pendekezo la Marekani, kwamba askari wenye silaha wawe wakisafiri katika ndege zinazoruka kutoka au kwenda Marekani, au hata zile zinazotumia anga la nchi hiyo kuelekea mahala pengine.

Msemaji wa shirika hilo Bwana Anthony Concil, amesema bila shaka shirika lake halina uwezo wa kuzuia uamuzi wa nchi fulani, inapochukua uamuzi wa aina hiyo, akasema kwamba hata hvyo shirika lake halikubaliani na wazo la kusafirisha askari wenye silaha katika ndege za abiria, huku akionya dhidi ya matokeo ya hatua hizo.

Bwana Anthony Concil pia amesema makambuni ya ndege hayawezi kulazimishwa kugharimia hatua hizo, zinapochukuliwa na idara za serikali. Akasema tangu yalipotokea mashambulio ya kigaidi ya september 11, 2001 nchini Marekani, makampuni ya ndege yamejitolea kuhakikisha usalama wa abiria, na kwamba serikali pia, ikiwemo serikali ya Marekani hazina budi kugharimia hatua zaidi za usalama.