Gazeti la Time lamtangaza Putin mtu bora wa mwaka 2007 | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 20.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Gazeti la Time lamtangaza Putin mtu bora wa mwaka 2007

WASHINGTON

Gazeti la Time nchini Marekani limemtangaza Rais Vladimir Putin wa Urusi kuwa mtu wake bora wa mwaka kwa mwaka 2007.

Gazeti hilo limesema uamuzi huo umetokana na jinsi Putin alivyoweza kuibadili Urusi kuwa muhimili muhimu katika karne ya 21.Limesema kuliko jambo lolote lile amepigania kuleta utulivu katika nchi ambayo takriban haukuwahi kushuhudiwa utulivu kwa mamia ya miaka.

Hata hivyo gazeti hilo halikusita kumkosowa kwa kusema kwamba Putin sio mwanademokrasia kwa kuzingatia hisia ya mataifa ya magharibi kwa neno hilo halikadhalika sio mfano bora wa uhuru wa maoni.

Ikulu ya Urusi ikizungumzia juu ya uteuzi huo imeuita kuwa ni kuungama juu ya dhima aliotimiza Putin katika kusaidia kuitowa Urusi kwenye vurugu za kijamii na kiuchumi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com