GAZA:Mzozo wa kisiasa waendelea Palestina | Habari za Ulimwengu | DW | 19.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA:Mzozo wa kisiasa waendelea Palestina

Wanachama wa Fatah na Hamas waliokuwa wametekwa nyara na watu waliokuwa na silaha wameachiliwa huru kufuatia mpango wa makubaliano ya amani kati ya makundi hayo mawili.

Wanaharakati wanane wa chama cha Fatah na wanne wa chama cha Hamas walikabidhiwa kwa wapatanishi wa makundi hayo.

Wakati huo huo waziri mkuu wa Palestina Ismail Haniyeh ambaye anashikilia msimamo wake wa kutokubali uchaguzi wa mapema anatarajiwa kutoa hotuba yake hii leo.

Hali ya wasiwasi kati ya makundi hayo mawili Hamas na Fatah imeongezeka baada ya rais Abbas kutangaza hapo jumamosi iliyopita kwamba kufanyike uchaguzi wa mapema ili kumaliza mivutano ya kisiasa iliyoibuka chini ya serikali inayoongozwa na chama chenye msimamo mkali cha Hamas.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com