GAZA: Wapalestina wawili wauwawa kwenye shambulio la jeshi la Israel | Habari za Ulimwengu | DW | 30.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: Wapalestina wawili wauwawa kwenye shambulio la jeshi la Israel

Wapalestina wawili wameuwawa kwenye shambulio la angani la jeshi la Isreal katika Ukanda wa Gaza usiku wa kuamkia leo. Duru za usalama za Palestina zinasema shambulio hilo liliilenga kambi ya wakimbizi ya Jabaliya kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Msemaji wa jeshi la Israel amethibitisha kwamba ndege za Israel zimewashambulia wanamgambo wenye silaha katika kambi hiyo ya Jabaliya lakini hakutoa maelezo zaidi.

Israel imekuwa ikizishambulia ngome za wanamgambo katika Ukanda wa Gza kwa wiki mbili kufuatia kuongezeka kwa mashambulio ya maroketi dhidi ya Israel yayonavurumishwa kutoka eneo hilo. Kufikia sasa wapalestina takriban 50 wameuwawa kwenye mashambulio hayo, wengi wao wakiwa raia.

Shambulio la usiku wa kuamkia leo limefanywa baada ya rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, kutangaza mipango ya kukutana na waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert kwa mara ya kwanza katika kipindi kinachokaribia miezi miwili.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com