GAZA: Wapalestina wawili washambuliwa na wanajeshi wa Israel | Habari za Ulimwengu | DW | 15.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: Wapalestina wawili washambuliwa na wanajeshi wa Israel

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Israel, kikosi cha jeshi la Israel kimewashambulia na pengine kuwaua wapalestina wawili karibu na eneo la mpakani kaskazini mwa Ukanda wa Gaza mapema leo.

Wanajeshi wa Israel waliwafyatulia risasi wapalestina hao walipokuwa wakiukaribia mpaka wakiwa wamebeba mabomu.

Maofisa wa Palestina hawajatoa taarifa yoyote kuhusiana na hatima ya watu hao. Usitishwaji wa mapigano baina ya Israel na Palaestina ulitangazwa majuma saba yaliyopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com