GAZA: Shambulio la Israel limeua Wapalestina 3 | Habari za Ulimwengu | DW | 20.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: Shambulio la Israel limeua Wapalestina 3

Shambulio la angani lililofanywa na Israel usiku wa leo limeua watu 3.Msemaji wa majeshi ya Israel amethibitisha kuwa gari la wanamgambo wa Hamas lililengwa katika shambulio hilo.Siku ya Jumamosi pia,Wapalestina 4 waliuawa katika mashambulio yaliyofanywa na ndege za kivita za Israel.Maafisa wa kijeshi wa Israel wanasema,ndege na vifaru vyake vitaendelea kuishambulia Gaza mpaka wanamgambo wa Hamas watakaposita kurusha makombora kusini mwa Israel.Kwa upande mwingine, makundi hasimu ya Wapalestina,Hamas na Fatah, yameanza kutimiza makubaliano mapya ya kuweka chini silaha katika Gaza na wamebadilishana kiasi ya wafungwa 30.Hilo ni jeribio la tano katika juma hili lililoshuhudia mapigano makali. Mapambano hayo yamesababisha vifo vya watu 51 na kuhatarisha serikali ya Wapalestina ya umoja wa kitaifa,iliyoundwa mwezi wa Machi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com