GAZA: Ngao ya binadamu imezuia shambulio la Israel | Habari za Ulimwengu | DW | 19.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: Ngao ya binadamu imezuia shambulio la Israel

Jeshi la Israel limezuia shambulio lililopangwa kufanywa na kikosi chake cha anga dhidi ya nyumba ya mwanamgambo wa Kipalestina.Hatua hiyo imechukuliwa baada ya majirani na jamaa wa Mpalestina huyo kukusanyika ndani na nje ya nyumba yake.Israel ilitoa onyo kwa familia ya mtu huyo kuashiria kuwa nyumba yao katika kambi ya wakimbizi ya Jabalya,kwenye Ukanda wa Gaza imelengwa kuteketezwa.Mwanamgambo huyo aliwaita majirani kuilinda nyumba yake kwa kujikusanya kama ngao.Jeshi la Israel limethibitisha kuwa limeahirisha shambulio hilo ili kuzuia majeruhi wa kiraia.Wakati huo huo,watu 6 wamejeruhiwa baada ya wanamgambo wa Kipalestina kuushambulia mji wa Kiisraeli wa Sderot kwa roketi zilizotengenezwa nyumbani.Mkazi mmoja amesema jumla ya roketi sita zilianguka katika mji huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com