1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA CITY, Wafanyikazi wa serikali Palestina walipwa mishahara yao

4 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBlu

Wafanyikazi wa serikali wanaomuunga mkono rais Mahmoud Abbas katika mamlaka ya wapalestina wameanza kulipwa mishara yao leo hii baada ya miezi 15.

Wafanyikazi hao wanalipwa kupitia benki zilizopo kwenye eneo la Gaza na ukingo wa magharibi.Hatua hii imechukuliwa baada ya nchi za magharibi pamoja na Israel kuahidi kumuunga mkono rais Mahmoud Abbas katika mzozo wa kuwania madaraka na kundi la Hamas ambalo linadhibiti kwa nguvu eneo la Gaza kuanzia mwezi uliopita. Hata hivyo rais Abbas amelitimua serikali kundi la Hamas na kusema wafanyikazi wote wa serikali wanaunga mkono kundi hilo hawatalipwa mishahara yao. Tangu kundi hilo la Hamas kuingia madarakani baada ya kushinda uchaguzi wa mwezi Marchi mwaka 2006 wapalestina 165,000 wafanyikazi wa serikali nusu yao wakiwa ni walinda usalama hawajawahi kupokea mishahara kufuatia jumuiya ya kimataifa kususia kuisaidia serikali ya Hamas.