Felix Magath-kocha mpya wa Schalke | Michezo | DW | 10.08.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Felix Magath-kocha mpya wa Schalke

Bundesliga imeanza kwa kishindo.

default

Felix Magath ushindi na Schalke ?

-Bundesliga imeanza kwa kishindo mwishoni mwa wiki huku Bochum ikitia mabao 3 mnamo dakika 12 kusawazisha mpambano wake na Borussia Monchengladbach.

Mabingwa mara kadhaa bayern munich, nusra wachezeshwe kindumbwe-ndumbwe na chipukizi Hoffenheim-timu iliozusha maajabu msimu uliopita.

-Dola kuu 3 za dimba barani ulaya lazima zitambe jumatano hii iwapo zinataka tiketi zao za Kombe liijalo la dunia huko Afrika kusini.

Tuanze na dimba:Bundesliga imerudi uwanjani mwishoni mwa wiki kwa msimu mpya na kama iliivyomalizika msimu uliopita,Wolfsburg iimeparamia tena kilelenii baada ya kuichapa Stuttgart mabao 2-0.

Mpambano uliokodolewa macho zaidi ilipoanza Bundesliga mwishoni mwa wiki ni ule kati ya mabingwa mara kadhaa-Bayern Munich na timu iliowasangaza mashabiiki wengi msimu uliopita-Hoffenheim.Munich iiliiokamia kufuta madhambi ya msimu uliopita,nusra ikione kiilichomtoa kanga manyoya pale bao Hoffenheim lilipokataliwa na rifu ingawa lilivuka chaki ya lango la Bayern Munich.

Laiti Hoffenheim iliokua ikicheza nyumbani ingekubaliwa bao hilo, basi pengine mpambano huo ungemalizika vyengine.

Mwishoe, lakiini ,Bayern munich iliondoka suluhu bao 1:1 na Hoffenheim.

kuhusu bao lililokataliwa la Hoffenheim, kocha wake Reinicke, alisema:

"Katika michezo mengine mfano Hoki ya barafuni,mpira wa kikapu-basketball,American football,zamani ushahidi wa video unatumika.Nadhani wakati umewadia kufanya hivyo pia katika dimba."

Kocha wa mabingwa msimu uliiopita VFL Wolfsburg, Felix Magath, aonesha amepania msimu huu kuitawaza Schalke 04 mabingwa.

Kwa mabao 2 ya Kevin kuranyi, Schalke imeilaza Nurmberg mabao 2:1.

Hamburg ilimudu suluhu ya bao 1-1 tu ilipocheza jana jioni na freiburg.

Msisimko lakini ulioonekana katika changamoto ya jana kati ya Bochum na Borussia Monchengladbach.

Bochum iliiiambia Borussia kutangulia si kufika na vishindo vyenu vya darini mwishoe, vitaishia sakafuni:

Borussia ilitangulia kutia mabao 3 kwa vishindo, lakini baadae ikaonekana kana kwamba wamechokoza nyuki.Kwani, Bochum walihitaji dakika 12 tu kusawazisha na kugawana pointi.

Baadae kocha wa Borussia Monchengladbach alisema:

"Kipindi cha kwanza tukiongoza wazi,lakini mtu avunjika moyo kutoka sare na kuondoka na pointi 1 tu."

Nae kocha wa Bochum iliotiia mabao 3 mnamo dakika 12 akasema:

"Nimewaambiia wachezaji wangu wacheze kwa ujasiri.Na baada ya kipindi cha kwanza kutoonesha ujasiri huo,kipindi cha pili walifanyahivyo walipocheza kufa-kupona."

Matokeo mengine ya Bundesliga ni kama hivi:Borussia Dortmund iiliitoa FC Cologne kwa bao 1:0 bao waliotia Cologne wenyewe langoni mwao.Werder Bremen iilizabwa mabao 3-2 na Frankfurt wakati bayer Leverkusen ilimudu sare 2-2 na chipukizi Mainz.

Dola 3 kuu za dimba kanda ya ulaya zitakuwa uwanjani jumatano hii kuania tiketi zao kwa Kombe lijalo la dunia:Ujerumani ina miadi na Azerbaijan.Ufaransa na Visiwa vya Faroe na croatia itafunga safarii hadi Belorusia.

Ujerumanii itaingia uwanjani mjini Baku bila ya Lukas Podolski, jogoo wa FC Cologne alieumia.Inatazamiwa lakini mshambulizi wa Taifa anaeichezea B.Munich Miroslav klose sasa ni fit kuikoa Ujerumani.Ushindi dhidi ya Azerbaijan utakiona kikosi cha kocha Joachim Loew ,kupanua mwanya wake kwa hadi pointi 4 kutoka Urusi kileleni mwa kundi la 4 kanda ya ulaya. Nahodha Michael Ballack atakuwa piia uwanjani baada ya stadi huyo wa Chelsea kuisaidia klabu yake kuitandika Manchester united jana katika mpambano wa ngao ya Community Shield.

Tumalizie mashindano ya Ubingwa wa Riadha ulimwengunii yanayoanza mwishoni mwa wiki ijayo mjinii Berlin:

Msisimko wa mashindano hayo yatakayoanza August 15 hadi 23, utakuwapo kwanza katika mbio za kasi za mita 100 na mita 200 ambamo bingwa wa olimpik na rekodi ya dunia Usain Bolt wa jamaica ana miadi ya changamoto na muamerika mweusi Tyson Gay.Mbio hizi ndizo zinazosubiwa mno mara tu kuanza mashindano haya mwishoni mwa wikii ijayo.

Katika changamoto ya mita 110 kuruka viunzi, bingwa wa Oliimpik na rekodi ya dunia kutoka Cuba Dayron Robels atazima vishindo vya wamarekani akiaahidi kurudi Havana na medali nyengine ya dhahabu.

Kuanzia masafa ya kati mita 800 hadi marathon nii kinyanganyiro cha waafrika wenyewe kwa wenyewe-Waethiopia,Kenya na wamorocco.

Bingwa wa olimpik wa mita 1.500 Rashid Ramzi wa bahrein amejitoa kwa kugunduzliwa na madhambii ya doping katika michezo ya mwaka jana ya olimpik mjini Beijing.

Mwengine atakaekosekana mjiini berlin, ni bingwa wa rekodi ya dunia aliyoiweka Berlin, muethiopia,mzee Haile Gebrselassie. Gebre ameam ua kutokimbia mara hii mjini Berlin na badala yake kukimbia mwezi mmoja baadae hapo septemba mbio za Berlin marathon.Katika mbio hizo ameweka rekodi za dunia 2007 na tena 2008.

Bingwa wa olimpik kutoka Kenya Sammy Wanjiru ameamua kuiandama rekodi ya muethiopia huyo kwa kushiriki katika Chicago marathon hapo oktoba 11.

Lakini, licha ya kujitoa kwa mabingwa hao, berlin itatawaza mabingwa wapya tangu upande wa wasichana hata wa wavulana.Usiache kuwa nasi kila siku kwa mapya kutoka Berlin juu ya mashindano ya 12 ya riadha ulimwenguni.

Muandishi: Ramadhan Ali/DPAE/AFPE

Mhariri: A.Liongo