Eneo la Shengen lapanuliwa | Habari za Ulimwengu | DW | 21.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Eneo la Shengen lapanuliwa

ZITTAU: UJERUMANI.

Viongozi wa Ulaya wamesherehekea kuondolewa kwa vizuizi vya mipaka katika eneo linalotoka katika bahari ya Baltic hadi maeneo ya Adriatic.Vizuizi hivyo vimeondolewa leo wakati nchi mpya zaidi katika umoja wa Ulaya, zilipojiunga na eneo lisilohitaji Passipoti la Umoja wa Ulaya.Kansela wa Ujerumani-Bi Angela Merkel, waziri mkuu wa Poland Donald Tusk na mwenzake wa Jamhuri ya Czech-Mirek Topolanek pamoja na rais wa Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso walikuwa wamepangiwa kusherehekea siku hii katika mji wa Zittau upande wa Ujerumani.Mji huo pia unazikutanisha nchi za Poland na jamhuri ya Czech. Sherehe hiyo ni moja wa sherehe kadhaa kwingineko katika ulaya katika kuzikaribisha nchi tisa, zamani zikiwa za kikomunisti, katika eneo linalojulikana kama la Shengen.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com