DUBAI : Al Qaeda kushambulia mafuta ya Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 15.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DUBAI : Al Qaeda kushambulia mafuta ya Marekani

Kitengo cha Al Qaida nchini Saudi Arabia kimetowa wito wa kushambuliwa duniani kote kwa mafuta yanayosafirishwa kupelekwa Marekani kwa kusema kwamba mashambulizi hayo sio tu yalenge Mashariki ya Kati bali pia Canada Venezuela na Mexico.

Tishio hilo la Al Qaeda limetolewa kwenye tovuti inayotumiwa na wanamgambo wa Kiislam.Kundi hilo lilikuwa limehusika na jaribio lililoshindwa hapo mwezi wa Februari mwaka 2006 kushambulia mtambo mkubwa kabisa wa kusafisha mafuta duniani wa Abqaiq nchini Saudi Arabia.

Maafisa na waratibu katika sekta ya mafuta na gesi nchini Canada wamesema wanaliangalia kwa makini tishio hilo lakini hawakuimarisha hatua za usalama.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com