Doa jeusi la Guantanamo nchini Marekani karibu kuondolewa | Matukio ya Kisiasa | DW | 19.12.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Doa jeusi la Guantanamo nchini Marekani karibu kuondolewa

Suala lililozusha utata la gereza la Guantanamo linatayarishiwa ufumbuzi hivi sasa.

Waandamanaji wakiwa wamevalia mavazi kama wafungwa wa jela ya Guantanamo wanapinga kuwasili kwa rais George W. Bush wakati alipofika kuhudhuria kikao cha mataifa ya Asia na Pacific APEC.

Waandamanaji wakiwa wamevalia mavazi kama wafungwa wa jela ya Guantanamo wanapinga kuwasili kwa rais George W. Bush wakati alipofika kuhudhuria kikao cha mataifa ya Asia na Pacific APEC.

Takriban miaka saba suala lililozua utata la gereza la Marekani la Guatanamo litakuwa limefungwa. Haya yamesemwa na waziri ambaye yuko hivi sasa madarakani na ambaye ataendelea kuwa waziri wa ulinzi Robert Gates. Rais mteule wa Marekani Barack Obama anatambua kuwa hiyo ilikuwa moja kati ya matamshi yake katika hotuba zake za kampeni na anafikisha mwisho hali ya mkanganyiko wa sheria za kimataifa. Lakini kuifunga jela hiyo inahitaji ushirikiano wa jumuiya ya kimataifa.


Mwanzoni kulikuwa na minyororo na vibanda vya nguzo za chuma, na baadaye kulikuwa na vyumba vya kisasa vyenye usalama wa hali ya juu. Kitu ambacho kinaendelea kuwapo baadaye ya miaka saba na kilichoukasirisha ulimwengu pamoja na watetezi wa haki za binadamu ni jela ambamo mfumo wa utawala wa kisheria unapindwa. Kutokana na hayo mtu anajaribu kupata kutoka kwa watuhumiwa wa ugaidi njia za kuhalalisha utesaji. Na kwa hiyo iwapo ni lazima kuwashtaki, tena mbele ya mahakama ya kijeshi, katiba na hatua za kisheria na utawala wa sheria nchini Marekani zitakuwa zinavurugwa. Utaratibu wa jela ya Guantanamo, ambao rais Bush baada ya shambulio la kigaidi mjini New York na Washington na kufuatia mapambano dhidi ya utawala wa Taliban nchini Afghanistan aliuanzisha , ni lazima ukomeshwe.

Wizara ya ulinzi ya Marekani ambayo ndio inadhibiti jela hiyo inatayarisha kufungwa kwake. Na kwa hiyo lile doa baya lililoichafua Marekani , huenda likaondolewa moja kwa moja.

Ni lazima nchi zote za kidemokrasia zinazofuata utawala wa sheria na watu wake wazifuate. Lakini tamko hilo la wazi halijatekeleza kitu chochote. Na hivi sasa ndio sababu hali hii inatakiwa kupatiwa ufumbuzi, na magaidi waendelee kukamatwa na kufikishwa mahakamani, watuhumiwa wa ugaidi wafikishwe mahakamani , lakini wale ambao hawana hatia wasibakie jela na waachiwe huru.

Ni mambo machache yangefanikiwa , iwapo rais mteule wa Marekani Barack Obama angeamua kulijenga upya jela la Guantanamo. Ama wafungwa, ambao hawana hatia wangeendelea kushikiliwa, ama kupelekwa katika nchi nyingine ambapo watatiwa kizuizini tena ama watakuwa katika hatari ya kuteswa. Hapa mataifa kama Ujerumani au mataifa mengine ya Ulaya yanapaswa kuchukua jukumu na mfano ni miongoni mwa kundi dogo la wafungwa wa Guantanamo wa kabila la Uigure, ambao ni Waislamu , ambapo mmoja wao alikuwa akifuatwa baada ya kuomba hifadhi nchini China.


►◄
 • Tarehe 19.12.2008
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GJvo
 • Tarehe 19.12.2008
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GJvo
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com