Dimba la olimpik | Michezo | DW | 31.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Dimba la olimpik

Klabu kadhaa zagomba kuwaachia mastadi wao kucheza katika olimpik Beijing.

Kabumbu ni mojawapo ya michezo ijayo ya olimpik inayoanza ijumaa ijayo mjini Beijing.Wakati katika kombe la dunia la FIFA,hakuna timu ya Afrika iliowahi kutawazwa mabingwa, michezo ya dimba ya olimpik yameshatawaza mabingwa 2 kutoka Afrika-nao Nigeria huko Atlanta,georgia,1996 na simba wa nyika-Kamerun katika michezo ya Olimpik ya 2000 mjini sydney,Australia.Brazil haikuwahi kutawazwa mabingwa wa Olimpik na mara hii imepania kufuta madhambi hayo.Ruhusa ya kucheza kwa mastadi wsake kama Ronaldinho wa AC Milan au Diego wa Werder Bremen imezusha utata na mvutano kati ya FIFA na klabu kama hizo.►◄

FIFA shirikisho la dimba ulimwenguni limetaka wachezaji wote chini ya umri wa miaka 23 waruhusiwe kuzichezea timu za nchi zao katika dimba la olimpik ambalo linajumuisha mara hii pia mabingwa 2 wa zamani waAfrika-Nigeria na kamerun pamoja na Ivory Coast.

Taarifa ya FIFA imesema na nakulu,

"kuruhusiwa wachezaji chini ya umri wa miaka 23 daima kumekuwa lazima kwa klabu zote kufuata.Na kanuni hii itatumika pia sasa huko Beijing." -alisema rais wa FIFA Sepp Blatter.

Ikasemekana kuwa Blatter ametuma barua kwa mashirikisho yote ya dimba kufuata muongozo huo.

Taarifa hii ilichomoza muda mfupi kabla klabu ya schalke ya Bundesliga hapa Ujerumani kutangaza kupeleka lalamiko lake kwa mahkama ya michezo kumzuwia stadi wake wa Brazil mwenye umri wa miaka 22 asiende Beijing.Hata umoja wa vilabu vya dimba vya Ulaya (ECA) ulidai pia klabu hizo haziwezi kulazimishwa kuwatoa mastadi wao wanaowahitaji mwanzo wa Ligi kwenda Beijing kwa olimpik.

Kwa kanuini, dimba la olimpik ni kwa wachezaji chini ya umri wa miaka 23,lakini ni ruhusa kwa kila timu kuingiza wachezaji 3 waliopindukia umri huo.Hawa si lazima kwa klabu kuwaruhusu kuondoka.

Mbali na klabu ya bundesliga ya Schalke, hata Werder Bremen ilisema kabla ya taarifa ya rais wa FIFA wangeweza kumzuwia Diego ambae hakupindukia umri wa miaka 23 kujiunga na Brazil huko Beijing.

Klabu ya barcelona katika la liga-ligi ya spian pia haikutaka kumuachia stadi wake kutoka Argentina Lionel Messi kuwachezea mabingwa wa Olimpik 2004.

Klabu hizo zikidai kwamba, mashindano ya dimba ya wanaume si sehemu ya kalenda rasmi ya mashindano kinyume na yale ya wanawake.Na kwahivyo, hazibidi kulazimika kuwatoa wachezaji wao.

Fikra hii pia ikiungwamkono na Shirikisho la kabumbu la Ujerumani DFB na hata Jumuiya ya klabu za dimba za ulaya ECA.

Hatahivyo, rais wa FIFA Blatter ameshikilia uzi wake ule ule aliposema kutojumuishwa dimba la olimpik katika kalenda ya mashindano ilifanywa makusudi ,lakini hii haina maana hakuna wajibu wa kuwaruhusu wachezaji kuzichezea timu zao katika olimpik.

Uchambuzi wa rais wa FIFA sepp Blatter unaungamkono ufafanuzi uliotolewa na Rais wa Halmashauri kuu ya olimpik ulimwenguni-IOC Jacques Rogge alieliambia shirika la habari la ujerumani DPA wiki iliopita kuwa wachezaji hao lazima waachiwe kucheza katika olimpik.

Klabu nazo zimeungama kwamba wachezaji wao wanashinikizwa mno kuwakilisha nchi zao katika olimpik.Brazil kwa mfano, ina uchu mkubwa wa kutawazwa mabingwa wa olimpik na kunyakua medali ya dhahabu ya dimba.Dola kuu maarufu za dimba za Ulaya hazishiriki katika dimba la beijing isipokua itali.

Klabu ya ujerumani iliopanda msimu huu tu daraja ya kwanza ilibidi kuridhia chipukizi wake Chinedu Obasi kuichezea Nigeria, mabingwa wa 1996 wa olimpik.

Wapi medali ya dhahabu ya dimba itaelekea mara hii ni vigumu kusema-Brazil lakini inadai kwa kila hali huu ni mwaka wake.