Condoleezza Rice: Siasa za Korea Kaskazini zitachukua mda mrefu kubadilika | Matukio ya Kisiasa | DW | 26.02.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Condoleezza Rice: Siasa za Korea Kaskazini zitachukua mda mrefu kubadilika

Waziri wa mambo ya nje nchini Marekani Condoleezza Rice amesema hatua ya Korea Kaskazini ya kuandaa tamasha lililoshirikisha bendi ya Philharmonic kutoka New York ni nzuri lakini siasa za nchi hiyo zitachukua mda mrefu k

default

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice na Rais wa China Hu Jintao


Waziri wa mambo ya nje nchini Marekani Condoleezza Rice amesema hatua ya Korea Kaskazini ya kuandaa tamasha lililoshirikisha bendi ya Philharmonic kutoka New York ni nzuri lakini siasa za nchi hiyo zitachukua mda mrefu kubadilika.


Vile vile Rice ambaye yuko ziarani barani Asia aligusia kwamba hivi karibuni itakuwa bora kuona wanafunzi wa kutoka Korea Kaskazini wakienda nchini Marekani kwa masomo zaidi.


Ni bendi ya Philharmonic kutoka New York nchini Marekani.


Bendi hiyo ambayo imekuwa ya kwanza kutoka Marekani kukubaliwa kutumbuiza mashabiki wa mziki nchini Korea Kaskazini ilipanda katika jukwaa lililopambwa kwa bendera za Marekani na Korea Kaskazini.


Kiongozi wa bendi hiyo Lorin Maazel alifurahisha mashabiki pale aliposema siku moja huenda mtunzi wa mziki akaandika wimbo unaitwa wamarekani walioko pyongyang.


Lorin amesema mwaliko waliopewa na Korea Kaskazini unaashiria uhusiano bora wa siku za usoni kati ya nchi hizo mbili.


Waziri wa mambo ya nje nchini Marekani Condoleezza Rice pia amepongeza mwaliko huo lakini akasema itachukua mda mrefu kwa nchi hiyo kubadili siasa zake.


Kufuatia mazungumzo yake na waziri wa mambo ya nje nchini China Yang Jiechi; Rice ameihimiza China kutumia kila iwezalo ili Korea Kaskazini isalimishe zana za Nyuklia.


Alipokutana na waziri wa nchi za nje wa China Rice alisema anaendelea kungojea Korea Kaskazini itangaze wazi mpango wake wa nyuklia kama ilivyoahidi mwaka jana.


Kwa upande wake Yang amesema China imekuwa katika mazungumzo na Korea Kaskazini na kwamba anatumai awamu ya pili ya magumzo hayo itafaulu katika njia zisizokuwa na upendeleo wowote. China imekuwa ikisaidia kuinua tena uchumi wa Korea Kaskazini ambayo ni marafiki wa tangu jadi.


Rice alisema hayo wakati bendi ya New York Philharmonic ilipoanzisha tamasha lake la kukata na shoka mjini Pyongyang kwa kucheza nyimbo za taifa za Korea Kaskazini na Marekani. Tamasha hilo linanuiwa kutengeneza uhusiano wa nchi hizo mbili.


Bendi hiyo ni ya kwanza kutembelea Korea Kaskazini na imeshuhudia ujumbe mkubwa zaidi kutoka Marekani ukikaribishwa katika nchi hiyo ambayo wakati mmoja mwaka wa 2002 ilitajwa na Rais George Bush kama kipengo chenye ufisadi.


 • Tarehe 26.02.2008
 • Mwandishi Mwakideu, Alex
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DDkU
 • Tarehe 26.02.2008
 • Mwandishi Mwakideu, Alex
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DDkU
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com