1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Die Linke

Chama cha mrengo wa kushoto (Die Linke) kilitokana na kuungana mwaka 2007, kati ya PDS kilichoithi chama tawala cha kikomunisti cha Ujerumani Mashariki (GDR) na WASG cha mrengo mkali wa kushoto cha Ujerumani Magharibi.

Kwa asili wapigakura wengi wa chama cha mrengo wa kushoto ni kutoka Ujerumani Mashariki, wafanyakazi na wazee -- ingawa katika siku za karibuni kimevutia pia wanachama wa SPD waliokatishwa tamaa. Wanakampeni dhidi ya kupunguzwa kwa malipo ya ustawi, lakini wanapigania kuwepo na kima cha chini cha mshahara na udhibiti mkali wa sekta ya benki. Ndiyo chama pekee cha Ujerumani kinachotaka kuondolewa mara moja kwa vikosi vya Ujerumani kutoka operesheni za nje na kuvunjwa kwa jumuiya ya NATO. Kikiwa na viti 63 kati ya jumla ya viti 631 baada ya uchaguzi wa 2013, chama cha Die Linke kinashika nafasi ya tatu kwa ukubwa, na ndiyo chenye nguvu zaidi katika upinzani. Ukurasa huu unakusanya maudhui za DW kuhusu chama hicho.

Onesha makala zaidi