Colombo:Waasi wa Tamil Tigers washambulia jeshi la serikali | Habari za Ulimwengu | DW | 28.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Colombo:Waasi wa Tamil Tigers washambulia jeshi la serikali

Jeshi la Sri Lanka limesema wanajeshi wake wameshambuliwa na waasi wa kundi la Tamil Tigers mashariki mwa nchi hiyo. Duru za kijeshi mjini Colombo zimesema, waasi walikua wakishambulia kwa mizinga mizito, na mwanajeshi mmoja aliuwawa na wengine watatu kujeruhiwa katika mapigano kwenye wilaya ya Batticaloa. Mapigano haya ya karibuni yametokea siku moja baada ya kiongozi wa ngazi ya juu wa waasi hao wa Kitamili, kusema usimamishaji mapigano wa 2002 sasa umevunjika. Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sri lanka vimewauwa zaidi ya watu 67,000 tangu 1983. watu 3,000 wameuwawa mwaka huu pekee.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com