COLOGNE: Washabiki wa kanivali wamiminika mitaani | Habari za Ulimwengu | DW | 11.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

COLOGNE: Washabiki wa kanivali wamiminika mitaani

Nchini Ujerumani,msimu wa kanivali umeanza leo hii,hasa katika miji iliyokuwa kando ya Mto wa Rhein.Washabiki,kwa maelfu wamekusanyika miji ya Cologne,Düsseldorf na Mainz ambayo ni ngóme za sherehe za kanivali.Mwezi wa Februari sherehe hizo zinafikia kilele chake.Wakati huo,watu wenye mavazi ya urembo na magari yaliopambwa huandamana barabarani katika sherehe kubwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com