China na Urusi zasisitiza uhusiano wao wa karibu
20 Mei 2026
Rais wa Urusi, Vladimir Putin anayefanya ziara nchini China amekutana na mwenyeji wake Rais Xi Jinping. Alipokelewa kwa shangwe na nderemo na mwenyeji wake Xi Jinping kwenye.
Kiongozi wa Urusi wakati wa mkutano huo mrefu uliofanyika siku ya Jumatano alipongeza 'misingi isiyotikisika' ya uhusiano wa pande mbili kati ya Urusi na China.
Viongozi wa Urusi na China wanatarajiwa pia kujadili maswala yanayohusu nishati na usalama miongoni mwa mambo mengine.
ambapo Rais wa China Xi Jinping mara baada ya kumalizika zoezi hilo la kutiliana saini alitahadharisha kuhusu dunia kurejea kwenye 'sheria za msituni' hiyo ni nahau inayoelezea mazingira ya ukatili ambapo sheria za kawaida, maadili, na ustaarabu havizingatiwi na badala yake mawazo ya wenye nguvu zaidi, maslahi yao binafsi na ubabe wao ndio huamua nani anayepaswa kupata mafanikio.
Rais Xi Jinping alimwambia mwenzake wa Urusi Vladimir Putin kwamba wao kama wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, nchi zao China na Urusi lazima zitimize majukumu yao kama mataifa makubwa, zidumishe mamlaka ya Umoja wa Mataifa kwa kusisitiza haki na usawa wa kimataifa.
Amesema China na Urusi zisimame kupinga uonevu na vitendo vyote vya kupendelea upande mmoja vinavyolenga kuigeuza historia ya dunia. Xi amesisitiza kwamba China na Urusi hasa zipinge vitendo vyote vya uchochezi vinavyolenga kuyakana mafanikio ya ushindi katika Vita vya Pili vya Dunia na hatua zinazojaribu kuubadili ulimwengu kwa kushinikiza ufashisti na nguvu za kijeshi.
Rais wa China amesisitiza kwamba ni lazima mataifa yote kwa pamoja yashirikiane katika kujenga mfumo wa utawala wa kimataifa unaozingatia misingi ya haki na usawa.
Rais wa Urusi Vladimir Putin yuko katika ziara ya kitaifa ya siku mbili nchini China inayokusudiwa kutilia mkazo uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Ziara hiyo ya kiongozi wa Urusi inafanyika siku chache tu baada ya ziara ya Rais wa Marekani Donald Trump nchini China.