1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama mshirika wa Merkel jimbo la Bavaria mashakani

Sekione Kitojo
14 Oktoba 2018

Wapigakura katika jimbo la Bavaria nchini Ujerumani wanapiga kura Jumapili (14.10.2018) ambapo chama hicho cha kihafidhina mshirika mkuu wa chama cha kansela Angela Merkel cha CSU kinaweza kupoteza kura nyingi.

https://p.dw.com/p/36WBb
Landtagswahl in Bayern Horst Seehofer 15.09.2013
Picha: Getty Images

Chama  cha  Christian Social Union , CSU, ambacho kimekuwa kikilitawala  jimbo  hilo bila  msaada  wa  chama  kingine  tangu mwishoni  mwa  miaka  ya  1950, kinatarajia  kupoteza  wingi  wake katika  bunge  la  jimbo  hilo, kwa  mujibu  wa  uchunguzi  wa  maoni.

CSU-Parteitag und Wahlkampfkundgebung
Mwenyekiti wa chama cha CSU katika jimbo la Bavaria Horst Seehofer katika mkutano wa kampeniPicha: picture alliance/AP/M. Schrader

Washirika  wengine  katika  muungano tete  wa  serikali unaoongozwa  na  Merkel , unaojulikana  kama  "muungano  mkuu" chama   cha  Social Democratic, SPD, pia  wanatarajiwa  kupoteza viti  vingi  wakati  chama  cha  siasa  kali  za  mrengo  wa  kulia kinachopinga  wahamiaji  cha  AfD kinaonekana kupata  uhakika  wa kuingia  katika bunge  la  jimbo  hilo.

Washindi  wakubwa  katika  uchaguzi  huo , hata  hivyo,  huenda wakawa  chama  cha  mrengo  wa  kushoto  cha  walinzi  wa mazingira , Greens  ambao  wameongeza  maraduru mvuto  wao kwa  wapiga  kura  hadi  asilimia  19  tangu  uchaguzi   wa  mwisho uliopita katika  jimbo  hilo, hali  inayoweza  kukifanya  chama  hicho kuwa chama  cha  pili  chenye  nguvu  katika  jimbo  hilo.

Watu  milioni  9.5  wenye  haki  ya  kupiga  kura  walitarajiwa kuingia  katika  vituo  vya  kupigia  kura  vilivyofunguliwa  asubuhi saa  12  kwa  saa  za  Ulaya  ya  kati. Iwapo uchunguzi  wa  maoni ya  wapiga  kura  utakuwa  sahihi, uchaguzi  wa  jimbo  la  Bavaria utaonesha  hatua  nyingine  katika kuporomoka  kwa  mwanvuli  wa vyama  vikubwa  na  kuvunjika  kwa uwanda wa  kisiasa , kama inavyoonekana  katika  mataifa  mengine  ya  magharibi.

Ludwig Hartmann und Katharina Schulze
Wagombea wa chama cha Kijani katika uchaguzi wa jimbo la Bavaria Katharina Schulze na Ludwig HartmannPicha: picture-alliance/NurPhoto

Kiongozi dhaifu

Kwa Merkel , ambaye  kwa  sasa  mara  kwa  mara  huonekana kama kiongozi  asiye  na  nguvu  tena  katika  muhula  wake  wa  nne madarakani  na  wa  mwisho, itasababisha  hali  ya  wasi  wasi  zaidi wa  kisiasa  wiki  mbili  kabla  ya  uchaguzi  mwingine  hata, katika jimbo  la  kati  la  Hesse.

Spika  wa  bunge la  Ujerumani  Wolfgang Schaueble , mshirika  wa muda  mrefu  wa  Merkel , amekiri  kwamba  uchaguzi  katika majimbo  hayo  mawili , utakuwa  na  athari  katika  siasa  za  taifa na  kuathiri  pia heshima  ya  kansela," ambaye  anawania kuchaguzi  tena  kama  mkuu  wa  chama  cha  Christian Democratic Union , CDU  mwezi  Desemba.

Chama  ndugu  cha  CSU  cha  jimbo  la  Bavaria  kwa  chama  cha Merkel  cha  CDU, kimekuwa  kwa  muda  mrefu  kikikumbatia  aina ya  siasa  za  kilabu  ya  pombe na  kudhibiti  madaraka  katika  jimbo hilo  linalofahamika  sana  kwa  kuwa  na  makasri, sherehe  za kunywa  bia  zinazofahamika  kam Oktoberfest, kamapuni  makubwa kama  Siemens  na  BMW pamoja  na  klabu  kubwa  tajiri  ya kandanda  ya  Bayern Munich.

Landtagswahl Bayern Horst Seehofer
Mwenyekiti wa chama cha CSU katika jimbo la Bavaria Horst Seehofer akimkumbatia kansela Merkel Picha: Reuters

Chama  hicho  kimekuwa  kikinadi  uthabiti  wa  kiuchumi  pamoja  na maadili ya  kihafidhina  katika  jimbo  hilo  amablo  wakaazi  wake wengi ni  Wakatoliki, wakihimiza  kuwapo  misalaba  katika madarasa ya  shule na  kupiga  marufuku uvaaji wa  hijabu hadharani  kwa  Waislamu.

Kama  chama  ambacho  kilikuwa  wakati  wote  kikipata  kura nyingi, chama  hicho  kutoka  katika  kile  kinachoitwa  jimbo  huru  la Bavaria  kimekuwa kikitawala kwa  pamoja  na  chama  cha  Merkel cha  CDU  mjini  Berlin katika  serikali  kuu.

Lakini  hali  hiyo  ilibadilika  baada  ya  katikati  ya  mwaka  2015, wakati  jimbo  hilo  linalopakana  na  Austria  ghafla  likawa  jimbo  la msitari  wa  mbele  nchini  Ujerumani  kwa  mmiminiko  wa  wakimbizi wengi  wao  wakiwa  Waislamu  na  mahamiaji wengine, nusu  yao kutoka  Syria , Iraq  na  Afghanistan.

Infografik Wenn heute Landtagswahl in Bayern wäre ... EN
Muonekano wa matokeo ya uchaguzi katika jimbo la Bavaria kutokana na uchunguzi wa maoni ya wapiga kura

Baada  ya hali  ya  awali  ya  kuwakaribisha , mmiminiko  huo ulizusha mapambano ya  chuki  dhidi  ya  wageni  ambayo yalisababisha  taifa  hilo  kujitokeza  kwa  chama  cha  AfD, ambacho katika  uchaguzi  mkuu  wa  mwaka  jana  kilichukua  mamilioni  ya wapiga  kura  na  kudhoofisha  vyama  vyote  vikubwa.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Yusra Buwayhid

Mhariri: Yusra  Buwayhid