CANBERRA: Howard ataka Umoja wa Mataifa uichukulie hatua kali Korea Kaskazini | Habari za Ulimwengu | DW | 09.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CANBERRA: Howard ataka Umoja wa Mataifa uichukulie hatua kali Korea Kaskazini

Waziri mkuu wa Australia, John Howard, amesema Umoja wa Mataifa utadharauliwa ikiwa hautatumia mamlaka yake kuichukulia hatua kali Korea ya Kaskazini kufuatia jaribio la nyuklia.

Aidha waziri Howard amesema Australia italitaka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lipinge utawala wa Korea ya Kaskazini ikiwa ni pamoja na vikwazo vya kifedha, usafiri na vikwazo vya kibiashara.

´Korea ya Kaskazini inafanya kosa kubwa ikiwa inafikiri jaribio lake la nyuklia litaipa uwezo mkubwa zaidi. Jaribio hilo limelitikisa eneo zima, na ni uvamizi wa usalama wa Korea ya Kaskazini. Inatakikana hatua kali ichukuliwe na jumuiya ya kimataifa na Australia itaiunga mkono kikamilifu hatua hiyo.´

Australia pia itafanikisha hatua za jumuiya ya kimataifa kupitia mashirika ya kikanda kama vile muungano wa nchi zinazosafirisha mafuta duniani, OPEC na baraza la kanda ya Asia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com