CAIRO : Wageni kadhaa mbaroni kwa njama za ugaidi | Habari za Ulimwengu | DW | 05.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CAIRO : Wageni kadhaa mbaroni kwa njama za ugaidi

Polisi ya Misri imewatia mbaroni Mmarekani mmoja, raia wa Ulaya 11 na watu wengine kadhaa kutoka nchi za Kiarabu kwa madai ya kula njama za kufanya mashambulizi ya kigaidi katika nchi za Mashariki ya Kati ikiwemo Iraq.

Taarifa ya wizara ya mambo ya ndani imesema hapo jana kwamba kundi hilo ni sehemu ya tawi la kigaidi la wanamgambo wa Kiislam ambalo limekuwa na mawazo ya itikadi kali na limekuwa likiishi nchini Misri chini ya kisingizio cha kuijifunza masomo ya Kiarabu na Kiislamu.

Miongoni mwa waliokamatwa ni Wabelgiji wawili,Wafaransa tisa na watu kadhaa kutoka Misri na nchi nyengine za Kiarabu zikiwemo Tunisia na Syria.

Taarifa hiyo imesema kwamba uchunguzi umethibitisha kwamba watu hao wana uhusiano na baadhi ya makundi ya kigaidi nchi za nje.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com