Bunge laidhinisha sheria ya kuwajumuisha wanachama wa Baath katika serikali. | Habari za Ulimwengu | DW | 13.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Bunge laidhinisha sheria ya kuwajumuisha wanachama wa Baath katika serikali.

Baghdad.

Bunge la Iraq limeidhinisha sheria ambayo inatoa nguvu ya kurejeshwa kwa waungaji mkono wa chama cha Baath nchini humo kushika nyadhifa katika serikali. Maafisa wa Marekani wamesema kuwa hatua hiyo ni muhimu kuelekea maridhiano ya kitaifa. Kura ilipigwa bungeni kwa kunyoosha mkono katika kila kifungu cha sheria hiyo yenye vifungu 30. Sheria hiyo ya uwajibikaji na sheria kama inavyofahamika rasmi, inataka kulegeza vikwazo kwa haki ya wanachama wa zamani wa chama cha Saddam Hussein kuweza kushika nyadhifa katika serikali.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com