Bunge la Senate kupigia tena kura mswada wa uchumi | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 01.10.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Bunge la Senate kupigia tena kura mswada wa uchumi

Bunge la Senate nchini Marekani limeafikiana kuupigia kura tena mswada unaolenga kuokoa soko la fedha.

Kiongozi wa chama kilicho na uwakilishi mkubwa kwenye Bunge la Senate Seneta Harry Reid

Kiongozi wa chama kilicho na uwakilishi mkubwa kwenye Bunge la Senate Seneta Harry Reid


Mpango huo unazimia kutumia dola bilioni mia saba kuiwezesha serikali kununua taasisi za fedha zinazokabiliwa na matatizo ya fedha.Kwa mujibu wa Kiongozi wa chama kilicho na uwakilishi mkubwa katika Bunge la Senate Harry Reid hatua hiyo imeungwa mkono na bunge hilo kwa minajili ya kuokoa uchumi wa Marekani.Rais George Bush kwa upande wake amesisitiza umuhimu wa kuchukua hatua za dharura.


Rais Bush alisisitiza kuwa lengo la hatua hiyo ni kulinda maisha ya raia wa Marekani.Hapo jana Baraza la wawakilishi la Marekani lilipinga mswada wa kuidhinisha dola bilioni mia saba kwa lengo la kuokoa jahazi la uchumi wa nchi hiyo.Mswada huo ulipingwa zaidi na wabunge wa chama cha Republikan.Bunge la Marekani Congress lilifungwa hapo jana kwasababu ya sherehe za mwaka mpya wa Kiyahudi Rosh Hashanah.

DW inapendekeza

 • Tarehe 01.10.2008
 • Mwandishi Mwadzaya, Thelma
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FS03
 • Tarehe 01.10.2008
 • Mwandishi Mwadzaya, Thelma
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FS03
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com