Mpango wa rais Bush. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 26.09.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Mpango wa rais Bush.

Mazungumzo ya kuutaua mgogoro wa fedha nchini Marekani yanaendelea Washington.

default

Rais G.W.Bush akiwa katika mazungumzo juu ya kuutatua mgogoro wa fedha unaoikabili Marekani.

WASHINGTON:

Mazungumzo juu ya  mpango  wa kutatua mgoro wa  fedha wa Marekani yataendelea leo.
Hapo  awali Seneta  maarufu  aliesema vyama  vyote  viwili vya  kisiasa  kwenye bunge  la Marekani  vinakubaliana kimsingi  juu ya  mpango wa rais  G. Bush wa kutenga dola BILIONI 700  ili kuifufua  sekta ya  fedha inayokabiliwa na  mgogoro mkubwa  nchini Marekani.

Seneta huyo Christopher Dodd , ambae ni mwenyekiti wa kamati ya baraza la seneti inayoshughulikia  masuala ya Benki ameeleza kuwa makubaliano ya kimsingi  yamefikiwa juu ya mpango huo. Seneta  Dodd anatumai  bunge litapitisha  sheria juu  ya mpango huo mnamo siku  chache zijazo.

Kabla ya hapo waziri  wa  fedha wa Marekani Henry Paulson alitoa mwito kwa wabunge wa vyama vya  Demokratik na Republican  kuwahimiza  waondoe tofuati zao haraka ili makubaliano yafikiwe kwa lengo  la kuyaokoa mabenki yaliyofilisika -  hali  inayotishia uchumi wa  Marekani kusababisha vurumai kwenye mosoko ya fedha  duniani kote.


Wakati  huo huo waziri  wa fedha  wa Ujerumani  bwana  Peer Steinbrüch amesema  Marekani  inaweza kupoteza nafasi yake kama  taifa kuu duniani, katika kuongoza mfumo wa fedha wa kimataifa   kutokana  na  mgogoro huo wa  fedha.

Akifafanua msimamo wa  nchi  yake juu ya mgogoro wa Marekani, waziri Steinbrüch  kwa mara nyingine amesistiza  mwito wake juu ya kuwepo udhibiti katika masoko ya  fedha  ya kimataifa.

Ameshuri haja  ya kupiga marufuku uchuuzi wa hisa wa harakaharaka. Waziri huyo wa Ujerumani ameeleza kuwa mgogoro  wa Marekani umesababishwa na uroho wa kutaka kujipatia  faida  katika asilimia za tarakimu mbili  pamoja  na bonasi kubwa zinazotolewa  kwa mameneja  wa mabenki.  

 • Tarehe 26.09.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FPJO
 • Tarehe 26.09.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FPJO
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com