BRUSSELS : Waziri Mkuu wa Ubelgiji akiri kushindwa
11 Juni 2007Matangazo
Waziri Mkuu wa Ubelgiji Guy Verhofstadt amekiri kushindwa katika uchaguzi wa bunge nchini humo.
Anatarajiwa kukutana na Mfalme Albert wa Pili leo hii kuwasilisha hati ya kujiuzulu kwa serikali yake mseto ya Waliberali na Wasoshalisti.Chama cha Christian Demokrat kimejizolea kura nyingi na wachunguzi wa mambo wanasema Guy Leterme kiongozi wa kitengo chao anayezungumza lugha ya Kiflemi anaweza kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo.
Inaweza kuchukuwa muda kidogo kabla ya serikali hiyo ya Ubelgiji kuundwa.
Huko nyuma ilichukuwa miezi minne kuunda serikali ya mseto ya vyama kutoka mikoa ya nchi hiyo inayozungumza Kiflemi na Kifaransa.