1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Suala la Kosovo kuamuliwa nje ya baraza la usalama.

21 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBge

Marekani pamoja na washirika wake wa mataifa ya Ulaya wameamua kuliweka suala la uhuru wa jimbo la Serbia la Kosovo kwa kundi la mahusiano la mataifa sita baada ya Russia kusema kuwa itapinga hatua hiyo katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya watalishughulikia suala hilo mjini Brussels siku ya Jumatatu na kundi la mataifa linalofanya mahusiano litakuwa na nchi za Uingereza, Marekani, Russia, Ufaransa, Itali na Ujerumani litakutana mjini Vienna siku ya Jumatano kwa ajili ya kushughulikia suala hilo.

Kundi hilo linalofanya mahusiano limetoa taarifa katika makao makuu ya umoja wa mataifa mjini New York kufuatia mazungumzo ya faragha ya baraza la usalama la umoja wa mataifa , ikisema kuwa imeamuliwa kuwa litatafutwa suluhisho nje ya umoja wa mataifa kwa ajili ya Kosovo. Russia haitakuwa na nguvu ya kura ya veto katika mjadala huo. Moscow imejiweka pamoja na Serbia , ambayo inapinga uhuru kwa jimbo hilo la Kosovo.