Brussels: Russsia inazishawishi nchi za Umoja wa Ulaya kuacha kuiwekea vikwazo serekali ijayo ya Wapalastina | Habari za Ulimwengu | DW | 28.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Brussels: Russsia inazishawishi nchi za Umoja wa Ulaya kuacha kuiwekea vikwazo serekali ijayo ya Wapalastina

Umoja wa Ulaya umesema kurejeshwa haraka misaada ya moja kwa moja kwa Wapalastina kunategemea mahitaji ya serekali mpya ijayo ya Umoja wa Taifa ya Wapalastina. Lakini Russia imeachana na msimamo wa nchi za Umoja wa Ulaya, na imesema itajaribu kuyashawishi madola ya Magharibi kuondosha vikwazo vya misaada kwa serekali ya Wapalastina inayoongozwa na Chama cha Hamas. Tangazo hilo limekuja wakati kiongozi wa Hamas, Khaled Meshaal, akitembelea Mosko ili kufanya mazungumzo na waziri wa mambo ya kigeni wa Russia, Sergei Lavrov. Madola ya Magharibi yanasema hayataondosha vikwazo vyao hadi pale Chama cha Hamas kitakapokubali kuitambua Israel, kuachana na matumizi ya nguvu na kuheshimu mikataba ya zamani na dola hiyo ya Kiyahudi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com