1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Angela Merkel asisitiza ushirikiano barani Ulaya

21 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGu

BERLIN

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel aliye pia kiongozi wa Umoja wa Ulaya kwa sasa anaonya dhidi ya mivutano barani Ulaya hususan kwenye suala la Marekani la kuweka kituo cha kupambana na mashambulizi ya makombora katika mataifa ya Poland na Jamhuri ya Czech.Akizungumza na gazeti la Rheinischen Post,Bi Merkel alisistiza kuwa Bara la Ulaya sharti liwe na makubaliano katika sera za kigeni na nishati.Nchi ya Mosco ambayo bado haijahusishwa katika majadilino ya mpango huo inapinga hatua hiyo.Marekani kwa upande wake inasema kuwa hatua hiyo inahitajika ili kupambana na tishio la mashambulizi kutoka mataifa kama Iran.