Baraza la usalama lashindwa kupitisha taarifa ya pamoja kuhusu Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 30.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Baraza la usalama lashindwa kupitisha taarifa ya pamoja kuhusu Gaza

Baraza la usalama la Umoja la Mataifa limekamilisha juma moja la mabishano na kuachana na juhudi za kuidhinisha taarifa ya pamoja kuhusu mzozo wa Ukanda wa Gaza.

Hatua hiyo inatokana na tofauti kati ya Libya na Marekani ambazo zimeshindwa kukubaliana juu ya vifungu vya maneno yaliyokuwa yatumiwe katika taarifa hiyo.

Wanachama 15 wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa walianza kujadiliana wiki moja iliyopita baada ya Israel kuvifunga vivuko vyake vya mpakani na Ukanda wa Gaza kuzuia mashambilio ya maroketi kutoka eneo hilo.

Hatua hiyo ilisababisha matatizo makubwa ya usafirishaji wa bidhaa za kiutu kwa wakaazi milioni 1.5 wa Gaza.

Balozi wa Libya katika Umoja wa Mataifa, Giadalla Ettalhi, ambaye ni rais wa baraza hilo kwa mwezi huu wa Januari, ameilaumu Marekani kwa mkwamo huo akisema imekataa marekebisho ya taarifa hiyo ya pamoja yaliyowasilishwa na Libya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com