Bara la Ulaya limefanya uchaguzi, lakini idadi ya waliopiga kura ni ndogo mno. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 08.06.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Bara la Ulaya limefanya uchaguzi, lakini idadi ya waliopiga kura ni ndogo mno.

Vyama vya kihafidhina katika bara la Ulaya vimepata ushindi katika uchaguzi wa bunge la Ulaya, huku Wasoshalist wakichukua nafasi ya pili wakifuatiwa na Waliberali na vyama vya mazingira.

Wafuasi wa chama cha CDU wakishangilia siku ya Jumapili 7. Juni 2009, katika makao makuu ya chama chao mjini Berlin baada ya kujulikana matokeo ya uchaguzi wa bunge la Ulaya.

Wafuasi wa chama cha CDU wakishangilia siku ya Jumapili 7. Juni 2009, katika makao makuu ya chama chao mjini Berlin baada ya kujulikana matokeo ya uchaguzi wa bunge la Ulaya.


Umoja wa Ulaya umechagua bunge jipya. Kwa kiwango kikubwa kabisa vyama vya kihafidhina vimeendelea kuwa imara zaidi katika bunge la Ulaya. Wasoshalist katika bara la Ulaya wamechukua nafasi ya pili, wakifuatiwa na Waliberali pamoja na vyama vya ulinzi wa mazingira , die Grünen.Kuporomoka kwa vyama vyote tawala , kupanda kwa vyama vyenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia na vyama vinavyotia shaka kuhusu umoja wa Ulaya pamoja na kujitokeza wapiga kura wachache , haya ndio mambo yaliyojitokeza zaidi katika uchaguzi huu wa bunge la Ulaya. Mara hii kwa jumla katika mataifa ya umoja wa Ulaya wamejitokeza wapiga kura asilimia 43 tu, ikiwa ni rekodi mpya yenye mwelekeo hasi kama alivyoeleza Marwick Kumalo ambaye alikuwa mtazamaji katika uchaguzi huu kutoka bara la Afrika.

Kile tulichokiona ni kwamba uchaguzi umetayarishwa vizuri kabisa, umekwenda vizuri, lakini kibaya katika uchaguzi huu ni juu ya kutokuwa na shauku ya kupiga kura, ina kera sana, amesema Kumalo.


Iwapo ni utawala unaofuata mrengo wa shoto kati , kama ilivyo nchini Austria, ama utawala wa mrengo wa kati kulia kama ilivyo Uholanzi, nchi zote hizi mbili ni mifano dhahiri ya mwenendo huu jumla. Kwa wapiga kura wengi wameziadhibu serikali zao na chuki dhidi ya wageni na vyama vinavyoukosoa umoja wa Ulaya vimesaidia kuleta hali hii.

Mporomoko mkubwa lakini umetokea nchini Uingereza, ambako chama tawala cha Labour baada ya kashfa ya matumzi ya wabunge kimeanguka.

Na kama ilivyo katika nchi kadhaa, pia matokeo hayo nchini Uingereza hayahusiki na siasa za Ulaya pamoja na mada za kitaifa.

Msisimko ulikuwa pia katika matokeo nchini Ireland kama ilivyotarajiwa, kwa kuwa mwishoni mwa mwaka huu Ireland itafanya pia kura ya maoni , kuidhinisha mkataba wa Lisbon. Watu wachache waliojitokeza katika uchaguzi nchini Ireland ama sehemu kubwa ya vyama vinavyopinga umoja wa Ulaya ilikuwa ni ishara mbaya.

Mgawanyo wa idadi ya wabunge katika bunge la Ulaya katika uchaguzi huu haukubadilika sana. Kwa jumla vyama vya kihafidhina vimeimarisha nafasi yao, bila shaka, ambavyo vimevitupa mbali vyama vya kisoshalist, ambavyo vimepoteza nguvu zao. Lakini pia vyama vya msimamo mkali wa kulia pamoja na wabunge wanaokosoa umoja wa Ulaya baada ya uchaguzi huu wataweza kutekeleza jukumu lao hilo muhimu.

Rais wa bunge la Ulaya Hans-Gert Pöttering ameeleza wasi wasi wake wazi wa ugumu wa kufanyakazi kwa pamoja.

Nina furaha kubwa, kwamba vyama vinavyopendelea umoja wa Ulaya vimepata wingi mkubwa, na nataraji pia kwamba vyama ambavyo havina msimamo huu , vitashiriki kwa pamoja katika bunge la Ulaya kwa mtazamo wa haki na kutoa mawazo yenye kujenga, na nawapongeza wabunge wote waliochaguliwa.Katika pande zote, wapiga kura wachache na kuongezeka kwa watu wa mrengo wa kulia pamoja na wakosoaji wa umoja wa Ulaya, kupata kwao idadi ya kutosha katika bunge ni mshtuko mkubwa. Katika siku zijazo itaonekana msingi wake, na kwa hiyo itawezekana kufanya tathmini.


Mwandishi Hasselbach, Christoph/ZR


Aliyetafsiri Sekione Kitojo.

►◄
 • Tarehe 08.06.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/I5TQ
 • Tarehe 08.06.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/I5TQ
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com