1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Umoja wa mataifa kutuma wajumbe kwenye mkutano wa usalama Iraq

1 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCNe

Umoja wa mataifa umesema utawatuma wajumbe wake maalum nchini Iraq katika mkutano wa usalama utakaofanyika mjini Baghdad mwezi huu wa Marchi.

Waziri mkuu wa Iraq Nuri al Maliki amesema anamatumaini kwamba mkutano juu ya usalama wa Iraq utafanikisha lengo la kuleta maridhiano na uungaji mkono wa serikali ya Iraq.

Maliki amezialika nchi jirani katika eneo hilo pamoja na mataifa yenye nguvu kwenye mkutano huo uliopangiwa kufanyika tarehe 10 mwezi huu.

Mkutano huo huenda ukafungua njia ya kufanyika mazungumzo kati ya Marekani na Syria pamoja na Iran.

Marekani inadai nchi hizo mbili ndizo zinazochochea ghasia nchini Iraq lakini nchi hizo zimekanusha madai hayo.

Marekani imesema itahudhuria mkutano huo huku afisa wa ngazi ya juu nchini Iran Ali Larijani akisema Tehran bado inatafakari pendekezo hilo.