BAGHDAD:Naibu Waziri Mkuu wa Iraq akoswa bomu | Habari za Ulimwengu | DW | 23.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Naibu Waziri Mkuu wa Iraq akoswa bomu

Naibu Waziri Mkuu wa Iraq wa kisunni Salam al Zubaie amejeruhiwa baada ya mlipuko uliosababishwa na mlipuaji wa kujitolea muhanga kwenye eneo la ulinzi mkali la Greenzone mjini Baghdad.Watu wengine wanane waliuawa akiwemo mshauri wake mmoja kulingana na polisi. Kwa mujibu wa mbunge wa chama cha Sunni Accordance Front,Dhafer al Ani,Bwana Zubaie yuko katika hali nzuri baada ya kufanyiwa upasuaji kuondoa mabaki ya bomu mwilini.

Mlipuaji huo alilipuka plae kiongozi huyo pamoja na Waziri Mkuu Nuri al MALIKI wakiwemo waumini wengine wakiondoka msikitini ulio kwenye uwanja wa nyumbani kwake.Kulingana na polisi gari moja lililoegeshwa karibu na hapo lililipuka wakati huohuo.Mshauri wa Bwana Zubaie aliyejeruhiwa alifariki baadaye akiwa hospitalini.Msikiti huo uko katika uwanja wa nyumba ya Naibu waziri mkuu huyo ila waumini wa nje wanaweza kuingia humo kwa swala.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com