1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Mshambuliaji wa kujitoa mhanga aua polisi 15

6 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4T

Watu 15 wameuawa na wengine 22 wamejeruhiwa baada ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga kujilipua nje ya kambi ya jeshi magharibi mwa Baghdad.

Waliyoauawa ni watu waliyokuwa wamejiandikisha kwa ajili ya kazi ya polisi kwenye jeshi la Irak.

Mshambuliaji huyo alijilipua akiwa katikati ya kundi la watu kwenye mji wa Abu Ghraib, na mashuhuda wanasema kuwa walinzi walimbaini lakini wakachelewa kumzuia asijilipue.

Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi hilo.Vikosi vya majeshi ya Irak vimekuwa vikishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa kisunni wakiwatuhumu kushirikiana na jeshi la Marekani.