BAGHDAD:13 wauawa kwenye eneo la Shuala | Habari za Ulimwengu | DW | 24.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:13 wauawa kwenye eneo la Shuala

Yapata watu 13 wameuawa katika mapigano ya hivi alfajiri kati ya wapiganaji wa Kishia na majeshi ya Marekani.Kwa mujibu wa maafisa wa afya na usalama,Dr Mohamed Abbas wa hospitali al Noor iliyoko magharibi mwa Baghdad wamepokea maiti 13 za watu waliouawa wawili kati yao wakiwa wanawake.Watu wengine 15 wamejeruhiwa na kupokelewa katika hospitali hiyo.

Kulingana na afisa wa usalama wa Iraq majeshi ya marekani yalipambana na wapiganaji hao mwendo wa saa tisa na saa kumi na moja alfajiri za Iraq.Wanajeshi hao waliwashambulia wapiganaji hao katika eneo la Shuala ambalo linadhibitiwa na jeshi la Kishia la Mahdi linaloungwa mkono na Moqtada al Sadr kiongozi wa kidini anayepinga marekani.Msemaji wa jeshi hilo Hamdallah al Rikabi alithibitisha kisa hicho lakini jeshi la Marekani halijasema chochote mpaka sasa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com