BAGHDAD: Waziri wa ulinzi wa Marekani ziarani Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 16.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Waziri wa ulinzi wa Marekani ziarani Iraq

Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates amekutana na Waziri Mkuu Nuri al-Maliki wa Iraq mjini Baghdad.Kabla ya mazungumzo yao,wanamgambo waliushambulia kwa bomu msikiti wa madhehebu ya Kisunni katika mji wa Basra ambako Washia wengi huishi.Hilo ni shambulio la pili la aina hiyo katika muda wa siku mbili.Inasemekana kuwa mashambulio hayo yanalipiza kisasi shambulizi la siku ya Jumatano lililosababisha uharibifu mkubwa kwenye msikiti wa madhehebu ya Kishia mjini Samarra.Waziri Gates anaefanya ziara ya ghafula nchini Iraq,hapo awali alisema,hakuridhika na mwendo wa pole pole wa serikali ya al-Nuri inayodhibitiwa na Washia,kujaribu kuleta upatanisho kati ya makundi hasimu nchini Iraq.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com