BAGHDAD: Waziri wa ulinzi wa Marekani afanya ziara ya ghafula Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 16.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Waziri wa ulinzi wa Marekani afanya ziara ya ghafula Iraq

Waziri wa ulinzi wa Marekani,Robert Gates amewasili mji mkuu wa Iraq,Baghdad kwa ziara ya ghafula na amekutana na makamanda wa majeshi ya Marekani.Alipozungumza na waandishi wa habari, Gates alisema,hakuridhika na utendaji kazi wa serikali ya Waziri Mkuu Nouri al-Maliki.Waziri Gates anatazamiwa kumuhimiza al-Maliki kujitahidi zaidi kuleta upatanisho kati ya jamii hasimu na kukomesha machafuko ya kimadhehebu na kushauri kuwa jamii zote zinufaike na mauzo ya mafuta.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com