1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Mkutano kutanzua mzozo wa kisiasa.

13 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZk

Waziri mkuu wa Iraq Nuri al Maliki anatarajiwa kuitisha kikao cha dharura mjini Baghdad, kwa lengo la kutanzua mzozo wa hivi sasa wa mkwamo wa kisiasa.

Moja kati ya malengo makuu ya waziri mkuu huyo ni kuwateua mawaziri wapya baada ya kundi la Wasunni Waarabu kujiondoa kutoka katika serikali yake ya umoja wa kitaifa. Waziri mkuu amesema kuwa anaweza akajaribu kuwataka kurejea katika serikali ama kutafuta Waarabu Wasunni wengine ambao watachukua nafasi yao.