1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ankara.Waziri Mkuu wa zamani wa Uturuki afariki dunia.

6 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvc
Rais George W.Bush akihotubia Bunge
Rais George W.Bush akihotubia BungePicha: AP

Waziri mkuu wa zamani wa Uturuki Bulent Ecevit, aliyekuwa kiongozi aliyeamrisha vikosi vya kijeshi kuivamia Cyprus mwaka 1974 amefariki dunia.

Ecevit alikuwa katika hali ya kutojitambua kwa muda wa miezi sita baada ya kupatwa na ugojwa wa kupooza tangu mwezi May.

Waziri huyo wa zamani alitawala kwa muda wa vipindi vitano akiwa kama waziri Mkuu Uturuki na aliku ni chachu ya siasa za kijeshi za Uturuki kwa kiasi cha miaka 50.

Kufuatia kipindi chake cha kwanza cha utawala Bulent Ecevit aliamrisha uvamizi wa Cyprus uliopelekea kugawika kwa nchi hizo hadi kufikia hii leo.