Ankara.Waziri mkuu wa Uturuki aanguka kutokana na kushuka kwa sukari mwilini. | Habari za Ulimwengu | DW | 17.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ankara.Waziri mkuu wa Uturuki aanguka kutokana na kushuka kwa sukari mwilini.

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, amekimbizwa hospitali mjini Ankara kwa matibabu, baada ya kuanguka na kupoteza fahamu.

Madaktari wamesema, waziri mkuu alikumbwa na matatizo ya kushuka kwa sukari mwilini, kulikosababishwa na funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani iliyomsababisha kuchoka sana, baada ya safari nyingi za kikazi.

Baadae televisheni ilimuonyesha waziri mkuu Erdogan akizungumza na madaktari Hospitali.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com