ANKARA: Mahakama ya katiba yachunguza ombi la upinzani | Habari za Ulimwengu | DW | 01.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ANKARA: Mahakama ya katiba yachunguza ombi la upinzani

Mahakama ya katiba nchini Uturuki inachunguza ombi la upinzani kupinga uhalali wa duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais nchini humo.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uturuki, Abdullah Gül, wa chama tawala cha AK, ambaye ni mgombea pekee wa wadhifa wa urais, alishindwa kupata thuluthi mbili ya kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo.

Jeshi la Uturuki na makundi mengine yasiyokumbatia sana maadili ya kidini nchini humo yanahofu kuchaguliwa kwa Abdullah Gül kutavunja makali sheria zisizo na misingi ya kidini.

Hapo awali mtaalamu wa sheria nchini Uturuki aliishauri mahakama ya katiba ikatae ombi la upinzani la kutaka uchaguzi wa rais ufutwe nchini humo. Mahakama hiyo inatarajiwa kutoa uamuzi wake hapo kesho.

Waziri mkuu wa Uingereza bwana Tony Blair ameitaka Uturuki iendeleze utawala wa kidemokrasia huku hali ya wasiwasi ikizidi kuhusu uchaguzi wa rais mjini Ankara.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com