Jumuiya ya kijeshi ya NATO imepata katibu mkuu mpya. Waziri mkuu wa Denmark
Waziri mkuu wa Denmark Anders Fogh Rasmussen amechaguliwa kuwa katibu mkuu mpya wa NATO.
STRASBOURG.
Viongozi wa NATO wamekubaliana kumchagua waziri mkuu wa Denmark ,kuwa katibu mkuu mpya wa jumuiya yao.
Televisheni ya Denmark imeripoti kuwa bwana Anders Fogh Rasmussen amechaguliwa baada ya viongozi wengine wa NATO kufanikiwa kuishawishi Uturuki.
Hapo awali Uturuki ilimpinga waziri mkuu huyo kwa sababu ya jinsi alivyoshughulikia mzozo juu ya kukashfiwa mtume wa dini ya kiislamu Muhammad katika vyombo vya habari nchini Denmark.
Katibu mkuu wa hadi sasa Jaap de Hoop Scheffer atajiuzulu mwishoni mwa mwezi julai.